Habari za Punde

Maulid ya Mtume Viwanja vya Maisara jana usiku


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akitia ubani kama ishara ya ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu
Ustadh Rashid Jaffer wa Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu.


Ustadh Abdulla Hamad wa Chuo cha Kiislamu,akitoa tafsiri ya Aya za Quran,zilizosomwa na Ustadh Rashid Jaffer wa Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Viongozi wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar,alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana, na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume,(katikati).[

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis,alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana
Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.