Habari za Punde

Waumini wa Kiislam Zanzibar Wahudhuria Maulid ya Kuzaliwa Mtume SAW.

 
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh Khamis Haji Khamis, akitowa maelezo kabla ya kuaza kwa Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kawa Mtume SAW yaliofanyika katika viwanja vya Maisara
 
 
Shekh. Mohammed Kassim wa Kamisheni ya Wakfu Zanzibar akisoma hutba ya kiswahili wakati wa sherehe za maulid ya kuzaliwa Mtume SAW yaliofanyika katika viwanja vya maisara na kuhudhuriwa na Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar


WANAFUNZI wa Madrasatul mbalimbali wakihudhuria  maadhimisho ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume (SAW) yaliofanyika kkitaifa katika viwanja vya Maisara,



 
   USTADH Waziri Hassan, akisoma mlango wa Dua ya Barzanji, ikiwa ni kuhitimisha maulidi ya kuzaliwa Mtume (SAW) yaliofanyika katika viwanja vya maisara na kuhudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Waumini wa Dini Kiislam. Yameadhimishwa kitaifa katika viwanja vya maisara Zanzibar
 Kutoka kulia Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhaj Amani Abeid Karume, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Khamis Haji Khamis, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Ali Mohamed Shein,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mufti wa Zanzibar Shekh. Saleh Omar Kabbi, walikimama kumsalia Mtume, wakati waMaulidi ya kuzaliwa Mtume SAW, yaliofanyika viwanja vya maisara. 
 Wananchi Waumini wa Dini ya Kiislam wakimsalima Mtume katikamaulid ya Kuzaliwa Mtume SAW, yaliofanyika katika viwanja vya maisara jana usiku.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh. Saleh Omar Kabbi, akisoma Dua kuhitimisha Maulid ya Kuzaliwa Mtume SAW, yaliofanyika kitaifakatika viwanja vya Maisara. Mjini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.