Habari za Punde

Ubuyu hupendwa na Watu Wengi kwa Sasa

Mti wa Mbuyu umekuwa kivutio cha Watalii wanaofika katika Visiwa vya Zanzibar na vitongoji vyake wanapokuwa katika matembezi yao sehemu mbalimbali za mjini na shamba,.katika visiwa hivi kama unavyooneka Mbuyu huu ukiwa katika moja ya Hoteli za Kitalii katika  ukanda ya Nungwi.
Ukiwa umepewa hifadhi nzuri na kuwa kivutio kwa Watalii wanaotembelea Hoteli hiyo .

Mabuyu kwa sasa katika visiwa vya Zanzibar na kwengineko yamekuwa mali kwa bidhaa hiyo kuwa ni moja ya malihafi katika kutengeneza vitu mbalimbali vya Kitalii na ubuyu wenyewe huwa ni moja ya kubudurisho hutumika. kwa kutengenezewa bidhaa mbalimbali kwa matumizi ya binadamu.

Pia tunda zake hutumika kwa kukamua mafuta kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa afya ya Binadamu na huongeza nguvu za kiume na kukuza virutubisho vya kinga mwilini na huleta faida kubwa kwa matumizi yake 


Ubuyu hutumika kama kiburudisho kwa wakati wa mapumzikohupikwa kwa sukari na rangi hupendwa na watu wengi katika visiwa vya Zanzibar na hata kusafirisha nje.Hutengenezwa juice kwa kutumia unga wake, tafautu na wakati wa nyumba enzi zenu ubuyu ulikuwa soko lake dogo kuliko sasa soko la ubuyu limekuwa kubwa na kufanya sehemu ya kituo hicho cha biasha hiyo kuwa na msongamano mkubwa.

Kwa hapa Zanzibar ukiuliza wapi uko ubuyu mzuri hupati tabu utaambiwa uko ubuyu mzuri Kiponda, na ukifika sehemu hiyo utakuta foleni kubwa wananchi wanataka bidhaa hiyo na haichukuwi muda unamaliza na kusubiri siku ya pili ukipikwa tena.

Ilibidi nifanye utafiti wa hali ya kudadisi biashara hiyo na kuambiwa biashara hii iko powa na kwa siku hupika kama kilo 100 hivi na wote husha na wateja wangu ni wengi ndani ya Zanzibar na Ughaibuni hupata oda nyingi.     .

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.