
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein, akitia saini kitabu cha maombolezi wakati alipofika kutowa salamu za mwisho kuuaga mwili wa marehemu Padri Evaristus Mushi katika kanisa la Minara Miwili wakati wa Ibada ya kuuombea iliofanyika katika kanisa hilo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein, akitoa salamu wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Padri Evaristus Mushi katika kanisa
la Minara Miwili wakati wa Ibada ya kuuombea iliofanyika katika kanisa
hilo 
Askofu wa Kanisa Katoliki Zanzibar Aguastino Shayo, akitowa
salamu zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Padri Evaristus Mushi katika kanisa
la Minara Miwili wakati wa ibada ya kumuombea.
MAANDAMANO ya Maaskofu wakiingia kanisani tayari kuaza kwa
Misa ya mkumuombea Padri Mushi katika kanisa Katiliki minara miwili jana.
ASKOFU Mkuu wa jimbo Kuu la Dar-es- Salaam Polycarp
Kardinali Pengo akiongoza Ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Padri Mushi
katika kisa iliofanyika katika kanisa la minara miwili jana. 
Askofu Banzi akifukiza Jeneza la Mwili wa Padri Evaristus Mushi wakati wa Ibada iliofanyika katika Kanisa Katoliki Minara Miwili Zanzibar. 
WAUMINI wa Kanisa Katoliki wakihudhuria misa ya Padri Mushi
kuuombea mwili wake katika kanisa la minara miwili jana kwa ajili ya mazishi
yaliofanyika katika eneo la Kitope.
Balozi wa Papa wa Kumi na Sita Tanzania akitowa Salamu za Papa wakati wa Ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Padri Evaristus Mushi, iliofanyika katika Kanisa Katoliki Zanzibar minara miwili. 
Askofu Banzi akiongoza Ibada wakati wa maziko ya kuuzika mwili wa marehemu Padri Evaristus Mushi katika maeneo ya Kitope nje ya Mji wa Unguja Mkoa wa Kaskazini. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Padri Evaristus Mushi. 
ASKOFU wa Kanisa Katoliki Zanzibar Aguastino Shayo akiweka
mchanga katika kaburi la Padri Evaristus Mushi . 
WATOTO wa Haki na Amani Jimbo la Zanzibar
wakiweka maua
kwa niaba ya watoto wezao wakati mazishi ya Padri Evaristus Mushi. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihudhuria mazishi ya Marehemu Padri Mushi katika makaburi ya Kitope Unguja. 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akihudhuria mazishi ya Padri Mushi.Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Juma Pembe, Waziri wa Mambo ya Ndani Dk.Nchimbi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis
No comments:
Post a Comment