RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kulia na CEO wa MCC, Daniel Yohannes, wakipiga makofi baada ya kuweka jiwe la msingi la Kituo Kikuu cha kupokelea Umeme Mtoni Zanzibar.ikiwa ni sherehe za uzinduzi wa Waya Mpya wa Umeme Zanzibar
Watoto wakiwa katika vyazi la Kanga ikiwa ni moja ya Vyazi la Zanzibar wakiwa wameandaliwa kwa ajili ya sherehe hiyo kutowamkasi wa kukatia utepe
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kushoto na CEO wa MCC Daniel Yohannes, wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kituo Kikuu cha Kupokelea Umeme Mpya kutoka Ras Kilomoni Dar-es-Salaam hadi kituoni hapo baada ya kupokelea katika kituo cha kwanza cha Ras Fumba Zanzibar.
MENEJA Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Mbarouk, akitowa maelezo ya mitambo ya kupokelea Umeme katika Kituo Kikuu cha Mtoni Zanzibar, kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein, baada ya kikizinduwa kituo hicho kipya.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto CEO -MCC Daniel Yohannes,, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Ardhi Makaazi ,Maji na Nishati Ramadhani Abdalla Shaban, wakiwa katika viwanja vya kituo kikuu cha umeme mtoni Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar MaalimSeif Sharif Hamad na Rais Mstaaf wa Zanzibar Amani Abeid Karume, wakiondoka katika viwanja vya Kituo Kikuu cha kupokea Umeme Mtoni baada ya kuzinduliwa na Rais wa Zanzibar.
NO RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. AliMohamed Shein na CEO – MCC Daniel Yohannes, wakizinduwa Umeme Mpya katika viwanja vya Amaan Zanzibar kulia Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Ramadhani Shaban na kushoto Meneja Mkuu wa ZECO Hassan Mbarouk. Wakishuhudia uzinduzi huo.
Viongozi wa Serekali wa kihudhuria sherehe za Uzinduzi wa Umeme Mpya katika viwanja vya Amaan Zanzibar, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, na Waziri wa Ardhi Makaazi, Maji na Nishati Ramadhani Abdalla Shaban.
Viongozi wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia Uzinduzi wa Waya Mpya wa Umeme katika viwanja vya amaan
WAFANYAKAZI wa ZECO na Wananchi wakishangilia uzinduzi wa Umeme mpya uliozinduliwa katika viwanja vya amaan na Rais wa Zanzibar .
JOPO la Wataalamu wa MCC wakifuatilia sherehe za Uzinduzi wa Umeme Mpya waya wake uliotandazwa baharini kutoka Ras Kilomoni Dar-es-Salaam hadi Ras Fumba Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar akizinduwa Umeme huo katika viwanja vya Amaan jana.
Super Kibonge, Halikuniki, Bery Black, DJ. Flash na Sultani Kingi wakiwa katika uzinduzi huo wakisubiri zamu yao kutowa burudani katika uzinduzi huo katika viwanja vya Amaan.
Wanafunzi walioandaliwa katika uzinduzi Waya Mpya wa Umeme wakiwa na mabovu ikiwa ni ishara ya uzinduzi huo.
Wasanii kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja Nungwi wakicheza Ngoma ya Mchikicho.
Wasanii wa Kikundi cha Mafunzo wakicheza Ngoma ya Kibati katika sherehe hiyo.
WASANI wa Kizazi Kipya Zanzibar Bery Black na Sultan King, wakitowa burudani katika uzinduzi huo wakishindikizwa na wasanii Super Kibonge na Halikuniki.
Viongozi wa Jukwaa kuu wakiitikia dua ikisomwa na Maalim Abubakary baada ya Uzinduzi huo .
Maali Abubakar akisoma dua baada ya Uzinduzi wa Waya Mpya wa Umeme uliofanyika katika viwanja vya Amaan Zanzibar.(Picha na Othman Maulid)
No comments:
Post a Comment