Habari za Punde

Uzinduzi wa waya mpya wa umeme ulivyofanyika Mtoni

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuzindua mradi wa Njia ya Pili ya Umeme, kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni, ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,hafla hiyo ilifanyika jana katika kituo kikuu cha Umeme Mtoni Mjini Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akikata utepe na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo, kama ishara ya uzinduzi mradi wa Umeme wa Njia ya Pili ,kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,hafla hiyo ilifanyika jana katika kituo kikuu cha Umeme Mtoni Mjini Zanzibar
  Hiki ni Kituo kikuu cha Umeme cha Mtoni Unguja.ambacho tayari Mradi wake uliofadhiliwa na MCC Marekani umezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,kwa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo, pia Balozi wa Marekani Nchini Tanzania ALfonso Lenhardt, alihudhuria katika uzinduzi huo,utakaochukua Ukubwa wa Kilowati 100


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo,(katikati) na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania ALfonso Lenhardt,wakipata maelezo ya kiutendaji kazi katika kituo kikuu cha umeme kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,kwa Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Ali,(kushoto)
baada ya ufunguzi rasmi leo,


Meneja Mkuu wa Shirikala Umeme Hassan Ali,(kushoto) akitoa maelezo kwa Viongozi mbali mbali walipotembelea Chumba Maalum chenye mashine za kupokea Umeme wa Njia ya Pili ,kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la
Marekani,akiwemo Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein

[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.