Habari za Punde

Uzinduzi wa waya mpya wa umeme ulivyofanyika uwanja vya Amaan

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) na wageni wake Balozi wa Marekeni nchini Tanzania Alfonso Lenhardt,na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo,pamoja na Viongozi wengine wakiangalia majarida yaliyocha pishwa kuhusu mradi huo wa Umeme wakati wa Sherehe zilizofanyika uwanja wa Amaan

 Baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Mji wa Unguja, wakiwa katika sherehe maalum za Uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Njia ya Pili kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,uliofadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,na akiwa Mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo, akitoa hutuba yake kwa Wananchi wa Zanzibar wakati wa Sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Njia ya Pili kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,uliofadhiliwa na Shirika la Misaada
la MCC la Marekani,sherehe hizo zilifanyika katika uwanja wa Amaan mjini Unguja
Balozi wa Marekeni nchini Tanzania Alfonso Lenhardt,akitoa hutuba yake kwa Wananchi wa Zanzibar wakati wa Sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Njia ya Pili kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni ,uliofadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,sherehe hizo zilifanyika katika uwanja wa Amaan mjini Unguja

Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.