Habari za Punde

Mtende Rangers yawika mjini


Na Mwajuma Juma
 
TIMU ya mpira wa kikapu ya Mtende Rangers, imezidi kudhihirisha kuwa ni moto wa kuotea mbali, baada ya juzi kuifunga Stone Town 90-89 katika mchezo wa ligi kanda ya Unguja kwenye uwanja wa Maisara.

Hata hivyo, haikuwa kazi rahisi kwa timu hiyo kushinda, ikipitwa mara kadhaa kwa magoli na wapinzani wao.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo uwanjani hapo kwa michezo miwili.

Pambano la kwanza litakuwa kati ya wapiganaji wa Nyuki a African Magic, huku majirani wawili, Mwembetanga na Mbuyuni wakitoana jasho baadae jioni.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.