Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel, Zanzibar-Mohamed Mussa akimkabidhi zawadi ya Modem ya 3G mmoja wa washindi wa promosheni ya 'Kwangua na Ushinde', bwana Simai Jarabu Idd
Washindi wa awamu ya kwanza wa promosheni ya ‘Kwangua na Ushinde’
ya Zantel iliyozinduliwa wiki iliyopita, wamekabidhiwa zawadi zao leo katika
kituo cha Huduma kwa wateja cha Zantel kilichopo Mlandege, Zanzibar.
Washindi waliokabidhiwa zawadi zao leo ni Bi Mwanamvua Suleiman
aliyejishindia muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni moja, Rashid
George aliyejishindia komputa ndogo ya Huawei pamoja na washindi wengine watano
wa 3G modem, Simai Iddi, Abdallah Juma, Subira Sheha, Zahor Mzee and Zainab Ali
Machano.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Mkurugenzi wa Biashara
wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa alisema zawadi hizo ni shukrani ya
kampuni ya Zantel kwa wateja wake zikiwa na lengo la kuwasaidia kiuchumi.
‘Zawadi hizi kwa wateja wetu zinadhihirisha nia ya kamupuni yetu
ya kuwawezesha wateja wetu kimaisha huku zikiwarahishia mawasiliano na ndugu na
jamaa zao’ alisema Mussa.
Promosheni ya ‘Kwangua na Ushinde’ ilizinduliwa wiki iliyopita na
mshindi mkubwa atajinyakulia zawadi ya gari huku washindi wengine wakijishindia
pikipiki, komputa ndogo za Huawei, modemu za 3G pamoja na muda wa maongezi wa
shilingi milioni moja.
Ili kushiriki katika promosheni hiyo wateja wa kampuni hiyo
wanapaswa kuweka muda wa maongezi wa shilingi elfu moja au zaidi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Pratap Ghose amewapongeza
wateja walioshinda zawadi hizo na kuwasihi waendelee kutumia huduma za Zantel.
‘Kampuni yetu ina dhamira kubwa ya kufanya huduma ya mawasiliano
inakuwa nafuu zaidi hapa nchini, na hiyo ni pamoja na kuboresha maisha ya
wateja wetu’ alisisitiza Pratap.
No comments:
Post a Comment