Habari za Punde

Balozi Seif amuaga Sheha wa Tomondo

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimuaga Sheha wa Shehia ya Tomondo Mohd Omar Said { Kidevu }  anayekwenda Nchini  India kwa Uchunguzi na Matibabu zaidi baada ya kumwagiwa Tindi kali usiku wa Tarehe 22 Mei 2013.
Sheha Kidevu alikuwa akipatiwa  huduma ya matibabu katika Hospitali Kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi mmoja baada ya tukio hilo.
Sheha wa Shehia ya Tomondo, Mohammed Omar Said Kidevu akitoa shukrani kwa SMZ kwa kufanikisha safari yake ya kwenda matibabuni  Nchini India mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ambae hayupo pichani wakati alipokwenda kumuuga rasmi kwa safari hiyo.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Bwana Mohd Omar Said { Maarufu Kidevu } ameondoka Zanzibar kuelekea Nchini India kwa ajili ya Uchunguz na matibabu zaidi baada ya kumwagiwa Tindi kali { Acid }  na mtu asiyejuilikana Usiku wa tarehe 22 Mei Mwaka huu wa 2013.
Sheha Mohd Kidevu alikuwa akipatiwa huduma zamatibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi Mmoja sasa kutokana na kuathirika sehemu ya kulia ya kifua chake, Bega pamoja na baadhi ya maeneo ya mapaja.
Mgonjwa huyo ameondoka na Ndege ya shirika la ndege la Oman kwa kupitia Muscut na amewasili Mjini Chenai Nchini India mapema leo tarehe 21/6/2013 saa 12.30 za asubuhi akiambatana na Daktari wake.
Akimuaga sheha huyo hapo katika wadi yake ya Mapinduzi Kongwe Mnazi Mmoja Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi alimuombea sheha Mohd Kidevu  safari ya mafanikio itakayomletea hafaja njema.

Bwana Mohd Kidevu alisema Mtu huyo alianza kutimua mbio baada ya kufanikiwa kufanya dhambi hiyo kitendo ambacho akalazimika kuomba msaada kwa wasamaria wema lakini hatimae ilishindikana kutokana na kuzidiwa kwa maumivu makali yenye kuchoma kama moto.
Sheha huyo wa Shehia yaTomondo aliendelea kumfahamisha Balozi Seif kwamba hali yake hivi sasa inaendelea vyema na ameshaanza kupata matumaini kufuatia jicho lake kuanza kuona ingawa bado anakabiliwa na maumivu katika sehemu yake ya usoni.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alimuomba Sheha huyo wa Tomondo kuwa na moyo wa subra wakati wa kipindi hichi kigumu cha huduma za matibabu.
Balozi Seif alimuhakikishia  Bwana Mohd Kidevu kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kufuatilia matibabu ya afya yake hadi atakapopata nafuu na kurejea nyumbani kuendelea na harakati zake za kimaisha kama kawaida.
Naye sheha wa shehia ya Tomondo Mohd Omar Said { Kidevu } aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada zake zilizosaidia kufanikisha kwa safari yake ambayo imempa faraja kubwa.
Sheha Kidevu alisema maumivu yaliyokuwa yakimkabili ndani ya wiki hii hasa wakati wa kula imepunguwa kidogo kufuatia huduma za karibu alizokuwa akipatiwa na madaktari wanaomuhudumia.
Akizungumza na vyombo vya Habari nje ya Wodi ya Mapinduzi Kongwe hivi karibuni wakati alipomkagua sheha huyo kwa mara ya kwanza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali  Iddi alisema Serikali Kuu imesikitishwa na vitendo hivyo viovu vinavyoleta athari kwa Binaadamu.
Balozi Seif alisema tabia hiyo mbaya inayoonekana kuanza kuchipua hapa Nchini ikibeba ufinyu wa imani inaanza kuleta hofu miongoni mwa wananchi katika kuendelea na harakati zao za kimaisha za kila siku.
Alisema Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi itaendelea na uchunguzi wa kufuatilia matukio hayo na kamwe haitasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa kuwafikisha katika mkondo wa sheria wale wote watakaobainika kuhusika katika vitendo hivyo.
Hili ni tukio la tatu kuwahi kutokea la kumwagiwa watu tindili kali ndan ya mkoa wa mjini Magharibi likiwahusisha aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Ndugu Rashid Ali Juma pamoja na Katibu wa Fufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Suleiman Soraga.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.