Habari za Punde

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Atembelea Watoto waliolazwa Hospitali ya Rufaa Mnazi mmoja.

 Jengo la Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mnazi Mmoja likionekana Pichani ambalo linatowa huduma kwa Wananchi wa Zanzibar kwa matibabu.   
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Tanzania Abdalla Majura Bulembo, akiongozana na Viongozi wa Umoja huo waliopo Zanzibar katika ziara ya kuwatembelea Watoto na wagonjwa wengine waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Abdalla Majura Bulembo, akimkabidhi zawadi mama wa mtoto aliyelazwa katika wodi ya watoto katika hospitali hiyo ikiwa ni ziara yake Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Wazazi Abdalla Majura akimsalimia mtoto aliyelazwa katika hospital hiyo. akiwa katika ziara yake Zanzibar.
 Kiongozi wa Wazazi Zanzibar Fatma Abeid akimkabidhi zawadi iliotolewa na Umoja huo kwa Watoto waliolazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.  

2 comments:

  1. Hawa jamaa hawana Nguo Nyengine zakuvaa Mpaka wavae Magandwa ya CCM na Mwenge.?

    Au ndio Waonekane kua wao ni CCM na Wanaimani sana na Wazanzibari?

    Ujinga mtupu wa hawa Mitwana kila unaemuona amevimba mpaka anataka kupasuka kwa Fitna, Rushwa, Uuwaji, ubaguzi, na Majungu. Rabi awaangamize mmoja mmoja na chama chao cha CCM kipite kiyayuke kama Moshi.. Chadema inakuja na Inawasomi wakweli kweli

    ReplyDelete
  2. Mimi kilio changu ni kwa akina Bora Afya na wenzake kwa kuigeuza CCM-Z'bar kua kikundi cha kutaftia kula.

    Matokeo yake sasa chama kinakufa huku wale waliokuaja kutafuta ajira (wadandia Basi) wanaangalia tu!

    Leo hii CUF inatamba huku wakiamua hatma ya Z'bar ktk muungano kana kwamba visiwa hivi ni vya kwao peke yao!

    Na kwa sasa hali ya CCM-Z'bar ni mbaya hawa jamaa wamepandikiza watu wa kutosha ndani ya CCM, sasa yameshakua yale ya URUSI NA GORBACHEZ!

    Nahodha pekee aiebaki na uchungu na mapenzi ya kweli na chama ni VUAI ..lkn. peke yake atafanyaje?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.