Mtume
Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam amesema:
{عليكم بقيام الليل فإنه دأب
الصالحين قبلكم، وقربة إلى الله تعالى، ومكفرة للسيئات، ومنهاة عن الإثم [رواه
أحمد والترمذي وصححه الألباني].
‘Ni wajibu kwenu kuuhuisha usiku kwa kusali kwani ( kufanya
hivyo) ni kuwaiga waliokuwa bora kabla yenu na kuwakurubisha kwa Allaah
Subhaanahu Wata’ala, na kuyatolea kafara (kusamehewa) madhambi na kuwakataza na
maasi na madhambi’
Imepokewa
na Ahmad na Attirmidhiy na Sheikh Albaani amesema ni
sahihi.
Sala
za usiku mkubwa (Tahajjud) zina fadhila nyingi na ambazo tukizikosa kwa
kutokutumia fursa hii adhimu na nadra ya kuzifanya ibada hizi basi tutakuwa ni
wenye kujutia katika maisha yetu.
Mtume
wetu Swalla Allaahu ‘Alayhi wasallam aliamrishwa na Mola wake kuamka usiku na
kusali na kupangiwa muda iwe nusu ya usiku au thuluthi ya usiku au azidishe
kidogo akisoma Qur’aan. ( Suuratu Muzammil 1-4)
Mtume
wetu ametuamrisha nasi tuzisali sala hizi kwa kujua umuhimu na fadhila zilizomo
ndani yake wakati Mola wetu hushuka hadi mbingu ya duniani na kuwatafuta wenye
kumuomba, wenye kufanya ibada, wenye kutaka msaada na kuwatakabalia maombi yao,
ibada zao na shida zao zote.
inshaallah atujalie wepesi juu yahili
ReplyDeletemwenyezi mungu atujaalie wepesi juu yahili.
ReplyDelete