Mtume
Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam amesema:
(إن الله وملائكته
يصلّون على المتسحّرين) رواه ابن حبّان
Hakika Allaah na
Malaika wake wanawasalia wanaokula daku
Imepokewa
na Ibn Hibaan
Kula
daku ni mojawapo katika mambo yaliyotiliwa mkazo na Mtume Swalla Allaahu ‘alayh
wasallam
Kwani
ndani yake kuna baraka na kheri nyingi , pia ni kujipamba na tabia za Mtume
wetu kwani jambo ambalo alikuwa akilifanya kila Ramadhaan. Tunapoamka kula
daku ni fursa ambayo Allaah Subhaanahu Wata’ala hushuka mpaka mbingu ya dunia na
kusubiri na kuwasikiliza wenye kuomba na
wenye shida zao awakubalie.
Tuitumie
fursa ya kula daku si kwa kula au kunywa pekee bali pia kwa kuomba maghfira kwa
Mola wetu na kwa lengo la kufuata Sunna ya Mtume wetu Swalla Allaahu ‘alayhi
wasallam.
No comments:
Post a Comment