Nyota Mpya Champions, Kundemba inatoa shukrani za dhati kwa Bwana Aboud Abdallah wa Copenhagen, Denmark kwa msaada wake kwa timu hii ambayo ipo daraja la Juvenile.
Msaada huu uliwasilishwa na Bwana Othman Ismail.
Msaada huo ukiwa ni mipira miwili mipya ya kiwango MITRE, Pump yake ya kutilia pumzi mipira MITRE na Collins English Dictionary kwa ajili pia ya mafunzo ya lugha kwa vijana wa Nyota Mpya Champions.
Bwana Aboud Abdulla ni mzanzibari anaeishi n'gambo, ni mdau wa mfuatiliaji wa karibu wa makala katika mtandao wa ZanziNews ambapo alisikia kilio chetu kupitia ZanziNews na kutuahidi kwamba atatusaidia mipira kwa ajili ya vijana wetu wa kesho.
Tunamtakia kila la kheri na mafanikio na moyo wa kuzidi kusaidia jamii.
Nyota mpya imelenga katika kuwaendeleza vijana hawa wanaoishi mtaa wa Kundemba kielimu pamoja na kimawazo na mtazamo kwa kupitia programu ya michezo.
Mtaa wa Kundemba ni miongoni mwa mitaa iliyoathirika vibaya na wimbi la madawa ya kulevya na hivyo uwepo watoto hawa katika mazingira hatarishi bila ya kuwa na mwongozo na mwelekeo kuna uwezekano mkubwa wa wao pia kuzama katika dimbwi hili la madawa.
Kama na wewe utakuwa umeguswa na programu hii na unataka kuchangia au kutaka maelezo zaidi tafadhali wasiliana na mlezi wa Nyota Mpya kwa namba ifuatayo +255 773 925313
Msaada wowote utapokelewa na kutumika katika malengo yaliyokusudiwa na si vyenginevyo.
NYOTA MPYA CHAMPIONS WAKIFURAHIA ZAWADI.
No comments:
Post a Comment