Habari za Punde

Sokoni Manunuzi ya Futari Zenji..

 Mambo ya ndizi kwa ajili ya futari chana moja inauzwa kati ya shilingi 4500/= na 2500/= katika soko la darajani.

 Kilo moja ya Tende huuzwa shilingi 4000/= bidhaa hiyo katika kipindi hichi hutumika sana kwa matumizi ya kufutaria wakati wa jioni.
 Mfanyabiashara ya futari ya Viazi Vitamu akipanga viazi hivyo kwa ajili ya Wateja wake viazi vitamu wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani hutumika sana kwa ajili ya futari fungu moja la viazi limauzwa shilingi 2000/= katika marikiti ya darajani.
 Wafanyabiashara ya Mbatata katika marikiti ya Darajani wakiwa katika harakati za biashara hiyo na wateja wao kilo moja ya mbatata inauzwa shilingi 750/= na vitunguu maji kilo moja shilindi 1600/=.
Mfanyabiasha ya bidhaa mbalimbali za Vyakula katika eneo la Rahaleo maarufu kwa biashara ya Mihogo mizuri iliyo na uhakika katika Zanzibar Regani akipanga Viazi Vikuu na maboga kwa wateja wake fungu moja ya la Viazi Vikuu likiuzwa kwa shilingi 2000/= na  boga kubwa shilingi 4000/=

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.