Habari za Punde

JK Amuondoa Naibu Katibu Mkuu Ujenzi.

Na Mwandishi wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemhamisha Mhandisi Ibrahim Iyombe, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wizara ya ujenzi.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema Eng. Iyombe anachukua nafasi ya Mhandisi John Stanslaus Ndunguru ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Aidha, taarifa imesema kuwa uhamisho huo unaanza mara moja.

1 comment:

  1. Jamani, tusione raha kuripoti ujasiri wa wenzetu tu ktk kuwajibishana, tutahamasishe hayo na kwetu Z'bar pia.

    Watu wengi wanapenda kutumia umahiri wa uongozi wa jamuhuri wakidhani hiyo ina 'impact' yoyote Visiwani lkn. sio kweli.

    Hata ktk vikao vya bunge lililopita, Mhe. Fenella Mkangara aliposema Tza ni ya pili Afrika, kusini ya jangwa la Sahara kwa kua na idadi kubwa ya magazeti na majarida viongozi wa SMZ walifurahi lkn. ukweli ni kwamba Z'bar bado ina gazeti moja tu!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.