Habari za Punde

Operesheni ya kuteketeza mifuko ya Plastiki, Pemba

 
POLO zilizopekiwa Vifuko vya Plastiki, vikishushwa kwenye Gari ya Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, kwa lengo la kuteketezwa kwa Moto, huko katika jaa la kutupia taka Vitongoji, vifuko hivyo vilivyokuwa na thamani ya Shilingi Milioni Saba (7), ambavyo vilikamatwa na kikosi kazi cha kudhibiti Uningizaji wa Mifuko ya aina hiyo kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman,Pemba.)

 
KIKOSI kazi cha kudhibiti uingizwaji na utumiaji wa Mifuko ya Plastiki Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakimimina vifuko vya aina hiyo huko kwenye jaa la kutupia taka Vitongoji, kwa ajili ya kuviteketeza kwa moto, vifuko hivyo vilikamatwa huko bandarini Wete, vikiwa katika polo  tisa (9) zenye kilo 477 na thamani ya shilingi Milioni Saba (7). (Picha na Abdi Suleiman,Pemba.)

 
KIKOSI kazi cha kudhibiti uingizaji na utumiaji wa  Mifuko ya Plastiki Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakivichawana vifuko hivyo kwa ajili ya kuviteketeza kwa moto, vifuko hivyo vilikamatwa huko bandarini Wete, vikiwa katika polo  tisa (9) zenye kilo 477 na thamani ya shilingi Milioni Saba (7). (Picha na Abdi Suleiman,Pemba.)

 
KIKOSI kazi cha kudhibiti uingizaji na utumiaji wa  Mifuko ya Plastiki Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakivichoma moto vifuko hivyo, huko katika jaa la kutupia taka Vitongoji, baada ya kukamatwa huko bandarini Wete, vikiwa katika polo  tisa (9) zenye kilo 477 na thamani ya shilingi Milioni Saba (7). (Picha na Abdi Suleiman,Pemba.)



VIFUKO vya plastiki vilivyokamatwa vikiendelea kuteketea kwa moto, baada ya kuchomwa na kikosi kazi cha kudhibiti uingizaji na utumiaji wa mifuko hiyo, huko katika jaa la kutupia taka Vitongoji. (Picha na Abdi Suleiman,Pemba.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.