Habari za Punde

Zoezi la Uboreshaji wa Daftari Awamu ya Pili

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akimkabidhi kadi ya Mpiga Kura Mkazi wa Kijiji cha Kimange Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani ambaye alifika katika kituo cha Shule ya Msingi Kimange kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mei 18, 2025. Jaji Mwambegele yupo mkoani Pwani kufuatilia mwenendo wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari awamu ya pili linaloendelea katika mikoa 16 ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. (Picha na INEC).
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akimwangalia Mkazi wa Fukayosi Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Bi. Siyani Ramadhani Waziri akisaini taarifa zake katika Kifaa cha Bayometriki ambaye alifika katika kituo cha cha Shule ya Msingi Fukayosi kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mei 18, 2025. Jaji Mwambegele yupo mkoani Pwani kufuatilia mwenendo wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari awamu ya pili linaloendelea katika mikoa 16 ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. (Picha na INEC).
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.