Balozi Seif akiagana na Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Kimataifa wa
Misaada wa Bill na Melinda Gates Bibi Arlene Mitchell mara baada yha mazungumzo
yao katika Ofisi ya Mfuko huo zilizopo kati kati ya Jiji la Seattle.
Kati kati yao ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko
Mh. Nassor Ahmed Mazrui.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia
kifaa kipya kabisa cha mawasiliano ya kompyuta Maarufu ipad kwenye kampuni ya
Microsoft akishuhudiwa na Waziri wa Biashara Kushoto yake Mh. Nassor Ahmed
Mazrui. Kulia yake ni Mtaa lamu wa Kompyuta wa
Kampuni ya Maicrosoft Mhandisi Daniel Moloznk na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akibadilishana mawazo na Mawaziri wake
aliofuatanao nao katika ziara yao
Nchini Marekani. Kushoto yake
ni Mh. Nassor Ahmed Mazrui Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko na kulia yake Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Znzibar Balozi Seif na Ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya
kuanza kutembelea ofisi ya Kampuni ya Microsoft kati kati ya Mji wa Seattle –
Washing Nchini Marekani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na ujumbe wake
akiangalia baadhi ya kompyuta mpya zilizoingia kwenye soko katika ofisi za
Kampuni ya Kimataifa bya Microsoft Mjini Seattle – Washington Nchini Marekani.
Balozi Seif akiwa katika
picha ya pamoja na Uongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa misaada wa Bill na Melinda
Gates pamoja na ujumbe aliofuatana nao mara baada ya mazungumzo yao kwenye
ofisi ya Mfuko huo Mjini Seattle
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Bingwa wa zamani wa Mbio za Magari Duniani Robert Shumake
aliyekuwa tayari kuingia ubia na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF }
katika mpango wake wa ujenzi wa nyumba za mkopo nafuu Mbweni,Robert Shumake
ni Ofisa Mkuu wa Taasisi ya Mtandao wa ushirikiano ya Latin America
iliyoanzishwa kwa lengo la kusaidia huduma za Kijamii kama
Ujenzi wa Nyumba, Afya pamoja na Elimu.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya Pamoja na Bingwa wa zamani wa Mbio za Magari Duniani Robert Shumake
kushoto yake mara baada ya
mazungumzo yao yaliyofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya Marriott Mjini
Seattle – Washington Nchini
Rais wa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima
Zanzibar Bw. Abdulla Abass akimpatia zawadi Maalum za Zanzibar Mkurugenzi Mkuu
wa kitengo cha Elimu ya Afya cha Microsoft Bwana Bill Crounse Mjini Seattle.
No comments:
Post a Comment