Habari za Punde

Makamo wa Rais Dkt. Bilal Ahudhuria Maadhimisho ya Wiki ya Mlipa Kodi Tanzania.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akihutubia wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam,leo,Okt 8, 2013.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti na zawadi, mshindi wa kwanza kwa kulipa kodi, Meneje wa Huduma za Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Alois Qande Maleck, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti na zawadi, mshindi wa pili kwa kulipa kodi,Mwakilishi wa Kampuni ya Sigara Tanzania, Paul Makanza, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Harry Kitilya, akimkabidhi Tuzo na Cheti, Mwananchi Shujaa wa Kodi, Dkt. Shumba,aliyediriki kuwekwa ndani kwa kudai Risiti ya malipo yake ya chumba cha Hoteli katika moja ya hotel katika mikoa ya Tanzania Bara, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo 
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Harry Kitilya, akimkabidhi zawadi na Cheti, Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibasila, Ally Mshana, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo

 Mshana akipokea Tuzo na Cheti kwa niaba ya Jukwaa la Wahariri.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.