Habari za Punde

Mwili wa Dkt. Sengondo Mvungi kuwasili KESHO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mwili wa Dkt. Sengondo Mvungi kuwasili KESHO (Ijumaa, Novemba 15, 2013) Saa 12:50 jioni

Alhamisi, Novemba 14, 2013


Tume ya Mabadiliko ya Katiba inawafahamisha wananchi kuwa mwili wa aliyekuwa Mjumbe wake ambaye alifariki nchini Afrika Kusini alikopelekewa kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi, Dkt. Sengondo Mvungi, unatarajiwa kuwasili nchini kesho (Ijumaa, Novemba 15, 2013) saa 12:50 jioni kwa Shirika la Ndege la Afrika Kusini.


Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu Dkt. Mvungi zimekamilika chini ya uratibu wa Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.


Baada ya kuwasili, mwili huo utapelekwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo iliyopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhifadhiwa. Marehemu Dkt. Mvungi ataagwa katika Viwanja vya Karimjee siku ya Jumamosi, Novemba 16, 2013.


Aidha, Marehemu Dkt. Mvungi anatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumapili, Novemba 17, 2013 kwenda Kisangara Juu, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu, Novemba 18, 2013.


Dkt. Mvungi alifariki siku ya (Jumanne, Novemba 12, 2013) katika Hospitali ya Millpark jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini alikopelekwa kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
Mwisho.

Imetolewa na:
Ndg. Assaa A. Rashid,
Katibu,
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.