Mtaalamu wa Huduma na Bidhaa wa Zantel, Bi Emmiliana Vakolavene akielezea huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni ya Zantel kwa washiriki wa shindano la Epiq Bongo Star Search. Kulia kwake ni Abdallah Sinani-Mkufunzi wa wataalamu wa Mauzo, na kushoto kwake ni Haji Yusuf, Meneja Kitengo Huduma za Ziada.
Mhamasishaji Jamii kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Malria, Makono Andrea, katikati, akizungumza na washiriki wa Shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search kuhusiana na mapambano dhidi ya Malaria. Kulia kwake ni Winnes Lyaro, balozi wa Malaria wa Zantel.
TARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
WASHIRIKI WA SHINDANO LA EPIQ BSS
WATEMBELEA OFISI ZA ZANTEL
·
Wapata semina ya Malaria, pamoja na matumizi ya
mitandao ya kijamii
Washiriki 6
bora waliobaki kwenye jumba la Epiq Bongo Star Search leo wametembelea ofisi za
Zantel ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo, ambayo
ndio wadhamini wa shindano hilo
kubwa la kuimba nchini.
Wakiwa ofisini hapo, washiriki hao ambao
walipata fursa ya kutembelea vitengo vyote vya Zantel na kuuliza maswali kwa
wakuu wa vitengo hivyo.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki hao,
mshiriki kutoka Mandela Nicholaus alisema lengo kubwa la ziara hiyo ni
kujifunza namna kampuni ya Zantel inavyotoa huduma zake.
‘Tumekuja hapa kujifunza namna kampuni ya
Zantel inavyofanya kazi lakini sambamba na hilo ni
kutoa shukurani zetu za dhati kwa udhamini wa Zantel kwenye shindano hili ambao
hakika umefanya shindano kuwa la kipekee sana ’
alisema Mandela.
Washiriki hapo pia walipata fursa ya
kujifunza kuhusiana na namna ya kupambana na ugonjwa wa Malaria.
Naye, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid
Khan akizungumza wakati wa kuwakaribisha washiriki hao kwenye ofisi za Zantel,
aliwapongeza kwa kuja kuwatembelea na kujionea namna wanavyofanya kazi.
‘Kwanza
niwapongeze kwa kufikia hatua hii ya sita bora kwani mmepita vikwazo vingi toka
usaili ulipoanza, na sisi Zantel tunaahidi kuwa tutaendelea kuwaunga mkono hata
baada ya mashindano haya kuisha’ alisema Khan.
Washiriki
waliotembelea Zantel ni Melisa John ambae namba yake ya kupigiwa kura ni 22, Amina
Chibaba (03), Emmanuel Msuya (21), Maina Thadei (15), Mandela Nicolaus (10) na Elizabeth
Mwakijambile (08).
Shindano
hilo ambalo sasa linafanya matamasha kwenye sehemu mbalimbali, ambapo wiki
iliyopita lilikuwa Temeke-Mwembe Yanga, na jumapili hii litakuwa Mbagala
viwanja vya Zakheem kuanzia saa nane mchana.
Kwa sasa, shindano la kuimba la Epiq BSS
liko katika hatua za mwisho, huku fainali yake ikitarajiwa kufanyika katika
ukumbi wa Escape hapo tarehe 30 mwezi wa kumi na moja.
No comments:
Post a Comment