Habari za Punde

Zanzibar Yalala dhidi ya Ethiopia kwa mabao 3--1

Timu ya Taifa ya Zanzibar imeshindwa kuonesha ubabe wake katika mchezo wake wa Pili wa michuano ya Kombe la Chalenhi kwa kufungwa na Timu ya Taifa ya Ethiopia kwa mabao 3--1mchezo uliofanyika katika uwanja wa Nyayo .

Timu ya Taifa ya Zanzibar imepoteza mabao mengi katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo na wapizania wao kutumia makosa wanaofanya wachezaji wa Zanzibar na katika kipindi cha kwanza katika dakika ya tano Ethiopia imeandika bao la kwanza kwa kupitia mshambuliaji wake aliounganisha mpira wa krosi.

Zanzibar itabidi ijilaumu kwa kupoteza mchezo huo kwa washambuliaji wake kuwa  butu wanapokaribia gali la wapinzani wao goli la Zanzibar limefungwa na Issa katika kipindi cha kwanza.

Ethiopia imefunga karamu ya mabao katika dakika ya 84 ya mchezo katika kipindi cha pili. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.