Habari za Punde

Mama Mwanamwema Shein akabidhiwa msaada wa fedha kwa vikundi vya jamii kutoka kampuni ya Sinohydro Tianjin Engineering ya China

  MKe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein, akimsikiliza Mkurugenzi wa   Sinohydro Tianjin Engineering Company ya China Bwa. Wang Jing Li, akitowa maelezo ya kampuni yao kabla ya kumkabidhi Cheki ya shilingi milioni tano kwa ajili ya Vikundi vya Jamii Zanzibar Makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Misali Sun Set Chakechake Pemba
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Sinohydro Tianjin  Engineering  Company ya China Bwa. Wang Jing Li, akitowa maelezo ya kampuni yao wakati wa hafla ya kukabidhi cheki kwa Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, kwa ajili ya Vikundi vya Jamii Zanzibar.
 WAKE wa Wawakilishi na Wabunge wakifuatilia hafla hiyo ya kukabidhiwa kwa cheki Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mama Mwanamwema Shein
 MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akikabidhiwa Cheki ya shilingi milioni tano na Mkurugenzi wa Kampuni ya Sinohydro Tianjin Engineering Company ya China, makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Misali Sun Set Pemba.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzzi Mama Mwanamwema Shein akisoma risala fupi kuishukuru kampuni ya Sinohydro Tianjin Engineering Company ya China baada ya kupokea cheki ya Milioni tano

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.