WAKE wa Wawakilishi na Wabunge wakimsikiliza Kiongozi wa Nyumba ya Sober house akisoma risala yao mbele ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na ujumbe wake aliofuatana nao katika ziara yake kisiwani Pemba.
MENEJA Msaidizi wa Sober house ya Mkoroshoni Mohammed Kassim akisoma risala kwa niaba ya Vijana wa Sober hiyo kwa Mke wa Rais wa Zanzibar na Ujumbe wake ulipofika katika nyumba hiyo kuwatembelea na kutowa misaada mbalimbali ya Chakula na sabuni kwa ajili ya Vijana hao. walioamua kuachana na matumizi ya dawa za kulevya
ACP Kheriyangu M.Khamis, Mkurugenzi wa Tume ya Uratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya, akitowa maelezo machache kuhusiana na hatua zinazochukuliwa kupambana na matumizi ya Dawa za Kulevya kwa Vijana na kutowa msaada kwa Vijana walioamua kuachana na matumizi hayo kwa kutowa ushauri nasaha.
VIJANA wa Sober House Mikoroshoni Chakechake Pemba wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, alipofika katika makazi yao kupata elimu ya kuacha matumizi ya dawa za kulevya hupata ushauri nasaha juu ya athari za matumizi yake.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi msaada wa Vyakula Kiongozi wa Nyumba ya Vijana walioachana na Matumizi ya Dawa za Kulevya Sober House ya Mkoroshoni Chakechake Pemba, ili kuwasaidia katika matumizi yao ya kila siku, makabidhiano hayo yamefanyika katika nyumba hiyo Mkoroshoni
No comments:
Post a Comment