Habari za Punde

Mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Mushi apewa dhamana


Mtuhumiwa wa Mauwaji ya  Padri Evaristus Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar Omar Musa Makame amepewa dhamana  katika mahakama kuu ya Zanzibar kutokana na kutokamilika kwa ushahidi wa kesi hiyo.
Akitoa dhamana hiyo Jaji Mkuu Omar Othman Makungu amesema mtuhumiwa huyo amepewa masharti mawili; moja kuwa atalazimka kupata wadhamini wawili watakoandika bondi ya laki tano  kila mmoja wakiwa na vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi (ZAN ID).

Na sharti la pili ni kuwa na barua ya sheha na kuripoti katika Mahakama mbele ya Mrajis Mkuu kila siku ya Jumatatu.

Mapema mwendesha mashitaka wa serikali, Abdalla Issa Mgongo alidai mahkamani hapo kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo kesi hio ipangiwe siku nyengine kwa kutajwa.

Nae kwa  upande wake Wakili anayesimamia kesi hiyo, Abdalla Juma aliomba Mahkama hiyo kuwa muda  umeshakuwa ni mwingi na  ushahidi bado haujakamilika hivyo ni vyema kesi hiyo kufutwa ikiwa haikuwezekana basi mtuhumiwa apatiwe dhana.

Kwa kuwa muda umeshakuwa mwingi na ushahidi hadi hii leo haujapatikana basi kesi ifutwe au Mtuhumiwa apewe dhama”alisema Wakili huyo Mahakamani hapo.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali Issa Mgongo alipingana na ombi hilo la kutaka kesi ifutwe na kusema ombi hilo hakubaliani lililotolewa na Wakili wa upande wa Mtuhumiwa.

Alisema ombi la pili lifanyiwe kazi likizingatiwa  mashati yatakayokubaliawa na mahakama.

Mtuhumiwa Omar Musa Makame  anadaiwa kumpiga risasi na kumuua Padre Mushi Februari 17 mwaka huu wakati akienda kuongoza Ibada ya Jumapili asubuhi katika kanisa la Mtakatifu Teresia liliopo Beit el Raas nje kidogo ya Mji wa Zanzibar . Alitiwa mbaroni Machi 17 mwaka huu.

http://zanzibariyetu.wordpress.com/
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.