Mtume
Swalla Allaahu ‘Alayhi Wasallam amesema
كفى بالمرء كذبا أن يحدث بكل ماسمع (رواه مسلم)
Yatosha kwa mja kuwa muongo akiwa ni mwenye kuhadithia kila analolisikia. Muslim
Muumini wa kweli hutakuwa kuwa na hadhari ili
asije kupigwa muhuri wa kuwa miongoni mwa wazushi. Kwani yanayosemwa kuna
yaliyo kweli na mengini si kweli. Hivyo ikiwa kila tutakalosikia tutalisema
tunaingia katika hatari ya kuwa miongoni mwa wanaosema uwongo.
Mwenye akili hufahamu kwamba si kila
analolisikia linapaswa kuhadithiwa.
Ndugu zangu katika imani, tukiletewa habari
yoyote ile kabla ya kuamua kuisambaza ni wajibu kwetu kuipima na kuiweka kwenye
mizani kama inafaa kuhadithiwa kwani habari yaweza kuwa ni kweli na sahihi
lakini haina faida wala maslahi kuhadithiwa. Inaweza kuwa ni ya uongo na haifai
kabisa kuhadithiwa kwa kuweza kuleta fitna na migongano.
Inaweza kuwa ni ya kutungwa na hivyo
kutuingiza katika kundi la wanaosambaza uwongo
na uzushi katika jamii.
Hivyo ni wajibu kwetu kuizingatia kwa
mazingatio makubwa hadithi hii ya Mtume wetu na Ruwaza yetu Swalla Allaahu ‘Alayhi
Wasallam hasa kwa tunaotumia mitandao iwe ya simu au ya intaneti, iwe ya blog
au kwenye facebook, iwe ya twitter au instagram, iwe ya whats up au skype na
mengineyo.
Tujichunge sana na kutuma au kusambaza habari
tu pasi na kuzingatia mafundisho ya Mtume wetu Swalla Allaahu ‘Alayhi Wasallam.
No comments:
Post a Comment