Na
Amina Omari, Kilindi
WAZEE
wa kimila wa kabila la kimasai, wameitaka serikali kuwashirikisha katika vita
dhidi ya ukeketaji wasichana na ndoa za umri mdogo.
Ushauri
huo umetolewa na kiongozi wa kimila wa jamii hiyo wilayani Kilindi mkoani Tanga,Simon
Oleamushana, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi.
Alisema
vita dhidi ya ukeketaji vitamalizwa iwapo viongozi wa jamii hiyo
watashirikishwa kwa ukamilifu wake.
Alisema
vita hivyo havitafanikiwa kwa kuwashirika watu wasiohusika na badala yake
kusikingizia kuwa wamasai hawataki kuachana na mila hizo.
“Najua
serikali inachukua juhudi kubwa kutaka kutokomeza mila za ukeketaji na mimba za
utotoni lakini wanachokosea hawatushirikishi sisi wazee wa kimila ambao ndio
tuna jukumu la kuleta mabadiliko katika jamii yetu,”alisema.
Nae
Raheli Ngushai alisema jamii hiyo imeonekana kusahauliwa katika mambo
mbalimbali ikiwemo elimu na afya hali inayosababisha kuendelea kushiriki
vitendo vya mila.
Hata
hivyo, aliyashukuru mashirika ya kijamii likiwemo AMREF kwa kujitolea
kuwaelimisha madhara ya ukeketaji kwa wasichana.
No comments:
Post a Comment