Habari za Punde

Ziara ya Waandishi wa Habari Kutembelea Ujenzi wa Barabara ya Maegesho ya Ndege na Kuondokea Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

Meneja Ufundi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Mzee Abdalla akiwaonesha waandishi mchoro wa  barabara ya kuondokea na maegesho ya ndege inayojengwa katikauwanja huokuweza kutumika kwa maegesho ya ndege kubwa kwa wakati mmoja, waandishi hao wamepata fulsa ya kutembelea miradi ya maendeleo ujenzi inayoendelea na ujenzi wake sehemu mbalimbali za Zanzibar 
Eneo la kuegesha ndege litakuwa na uwezo wa kuchukuwa ndege kubwa na zaidi ya tano kwa wakati mmoja likiwa katika hatua ya kuwekwa lami wakati waandishi Zanzibar na Tanzania Bara kutembelea miradi ya Maendeleo Zanzibar.
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, akitowa maelezo kwa waandishi wa habari walipofanya ziara kutembelea uwanja huo na kujionea mradi wa barabara ya kuondokea na ujenzi wa maegesho ya ndege  uwanjani hapo.
Waandishi wakiwa katika uwanja wa ndege wakioneshwa sehemu mbalimbali za uwanja huo unavyoendelezwa kwa ujenzi wake na kufikia kiwango cha hali ya juu katika huduma yake ya usafiri wa ndege
Hili ni jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume linalotarajiwa kuaza tena ujenzi wake hivi karibuni na kukamilika kwake linauwezo wa kutowa huduma kwa wasafiri zaidi ya watu 1000 kwa wakati mmoja kupata huduma za usafiri wa kimataifa kuptia jengo hilo.
Sehemu ya maegesho ya ndege za abiria likiendelea na ujenzi wake kwa kuweka lami laini ikiwa hatua ya mwazo 

                                   Eneo la chumba cha abiria wanaoondoka Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.