Habari za Punde

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania JK Apokea Matembezi ya Vijana Maisara

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania kihutubia katika maadhimisho ya Matembezi ya Vijana wa CCM baada ya kutembea katika Wilaya zote za Unguja na Pemba kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi na kuwaenzi Wazee wa liopigania Mapinduzi ya Zanzibar.
Mwenyekiti wa UVCCM na Mbunge wa Donge Mhe. Sadifa akihutubia katika mkutano wa mapokezi katika viwanja vya maisara.
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka akisoma risala ya Vijana katika maadhimisho ya matembezi hayo baada ya kupokelewa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Kikwete.
 Viongozi wa CCM wakifuatilia hutuba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Kikwete akihutubia katika viwanja vya Maisara.
Vijana wa UVCCM Walioshiriki matembezi  ya Kuwaenzi Wazee Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia baada ya kupokea matembezi hayo katika viwanja vya Maisara. 
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea saluti kutoka kwa Vijana wa Chipukizi walioandaa bwaride maalum kwa ajili ya mapokezi hayo ya Matembezi ya kuwaenzi Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi.katika viwanja vya Maisara 
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akikagua Bwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili ya mapokezi ya Vijana wa UV CCM wanaoshiriki matembezi.

Wananchi wakifuatilia matembezi hayo katika viwanja vya maisara yalikomalizia matembezi hayo, yaliaza kisiwani Pemba katika Wilaya ya Micheweni na kumalizia Wilaya ya Mjini Unguja.Viongozi wa matembezi ya kuwaenzi Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar wakipita mbele ya Mgeni rasmin 
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipokea Matembezi ya Vijana wa UVCCM katika viwanja vya maisara kukamilisha matembeziyao waliotembea katika Wilaya zote za Unguja na Pemba. 
Waasisi wa Umoja wa Vijana wa ASP wakipita mbele ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, wakikumbuka enzi zao wakiongozwa na Mzee Aboud Talib na Mzee Ramadhani Makweya. 

Vijana wa matembezi ya kuwaenzi Viongozi waliopigania Mapinduzi ya Zanzibar wakimalizia matembezi hayo katika viwanja vya maisara.
                        Watangazaji wa ZBC wakihabarisha wananchi waliokosa kufika katika viwanja hivyo.
Kikosi cha Bendera kikitowa heshima katika bwaride hilo maalum kwa ajili yaMapokezi ya Matembezi ya Vijana wa UVCCM katika viwanja vya Maisara.
             Mambo ya enzi zile za  Paunia katika viwanja vya yuthiligi na lkumalizi maisara ilikuwa kama hivi.
Vijana wa Chipukizi wakiinua mguu katika bwaride hilo maalum la kupokea Matembezi ya Vijana wa UVCCM kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vijana wa Chipukizi wakipita kwa mwendo wa haraka kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya Maisara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.