Hivi ndivyo utakavyokuwa Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi unaojengwa katika viwanja vya Michezani Unguja Zanzibar.
Hatua ya mwazo ya ujenzi wa mnara huo inaendelea na ujenzi wake unaojengwa na Kampuni ya CRJE ya China.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mshauri Ujenzi wa Mnara huo Bwa Habibu Nuru, wa Kampuni ya Hab Consult, alipofika kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mnara huo unaojengwa katika maeneo ya Michezani Kisonge Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la Mnara wa kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Viongozi wengine wakifurahia uwekaji wa jiwe hilo la Msingi na Rais wa Zanzibar.
Mshauri Ujenzi wa Kampuni yaHab Consult, Bwa. Habibu Nuru, akitowa maelezo ya michoro ya Mnara huo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Ujenzi wa Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, unaojenwa katika viwanja vya michezani kisonge.
Wafanyakazi wa ZSSF wakifuatilia sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi
upotevu wa fedha za umma kwa kitu kisicho na manufaa kwa binadamu , wakati nchi inahangaika haina vitu muhimu vya maisha, sijui wawakilishi wanasinzia huwa hawaoni , au ni akili finyu
ReplyDeletesawa ila hizi project ziendelee musije kutuachia magofu na nyengine zikabaki makaratasini,maana airport mumetuachia frame mpk leo
ReplyDeleteHongera marehemu ASP na hongereni wale wote wenye itikadi za ASP maana mnara wa kumbukumbu kujengwa Kisonge kweli panastahiki au ni mbinu za wachache tuu. Kwani kuna masuala la kujiuuliza hapo,jee hapo unapojengwa ndipo palipopangwa Mapinduzi? Au hapo ndipo palipodata sisasi ya mwanzo ya mapinduzi? Au hapo ndipo palipotumika panga au mchale wa mwanzo katika kuhujumu siku ile? Mie naona watamke tu moja kwa moja kuwa hapo ndipo kilipoundwa chama kilicholeta mapinduzi. Kisonge hapana umuhimu wowote na mapinduzi kwa mantiki ya miaka 50. Ilikuwa muulize na mpate maoni ya watu kwanza ,Arusha pana mnara wa azimio la Arusha.Kisiwandui pana sanamu la Karume panastahiki lakini Kisonge mnawaziba macho tu wasioona ili wazidi wasione.
ReplyDeletemchangiaji maalim seif yupo pale
ReplyDeleteHapana mahusiano yoyote mnara wa miaka 50 ya mapinduzi kujengwa kisonge kwani hapo ndipo palipopangwa mapinduzi au hapo ndipo palipodata risasi ya mwanzo siku ile au hapo ndipo paliporushwa mshale wa mwanzo au hapo ndipo palipokuwa ni kituo cha mwisho kusalim amri na mapinduzi yakawa yamefanikiwa? Mie naona it is a wrong place.
ReplyDelete