Habari za Punde

Majaji tunzo ya EJAT waapishwa

Na Fatuma Kitima, DSM
RAIS wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jaji Robert Kisanga, amewapisha majaji wa tunzo ya uandishi mahari wa habari (EJAT) 2013 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuanza kupitia kazi zilizowasilishwa kushindaniwa na waandishi wa habari.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT 2013, Kajubi Mukajanga, alisema walioapishwa ni Gervas Moshiro ambye ni Mwenyekiti wa jopo hilo,Mwanzo Milinga,Pudenciana Temba, Hassan Abdallah Mitawi,Ananilea Nkya,Jesse Kwayu,Pili Mtambalike,Chrysostom Rweyemamu na Suleiman Kissoky Mjumbe.

Mukajanga alisema baada ya mchakato wa kuapishwa majaji hao, kinachofuata ni kumtafuta mshindi wa tunzo za maisha ya mafanikio katika uandishi wa habari.

Alisema tuzo hizo zitatolewa kwa kumtambua mwandishi ambaye katika maisha yake ametoa mchango mkubwa kuendeleza tasnia ya habari nchini.


Aidha alisema utaratibu wa kumtafuta mshindi wa tuzo za maisha ya mafanikio katika uandishi wa habari ni toafauti na wa EJAT ambapo washindi wanatokana na makundi mbalimbali ya kusindaniwa.

Alisema mchakato huo unahusisha jopo la wataalamu ambao huandaa orodha ya waandishi na maelezo kuhusu maisha yao ikiwemo kuchambua mmoja hadi mwingine huku wakizingatia vigezo vilivyoandaliwa na EJAT.

Alisema jopo hilo la wataalamu mwishoni litateuwa majina matatu yenye sifa kwa ajili ya kuwasilisha kwa wakuu wa wataasisi za kihabari washirika wa EJAT ambapo humchagua atakayekuwa mshindi.

Aidha alisema jopo la wataalamu wa tunzo za maisha ya mafanikio katika uandishi wa habari linaongozwa na Mwenyekiti, Theophil Makunga, mwandishi mzoefu Jenerali Ulimwengu, Lillian Kallaghe, Hamis Mzee na Joyce Mhavile.

Jumla ya kazi 907 za kushindaniwa katika tuzo za umahiri wa uandishi wa habari 2013 zimewasilishwa idadi ambayo ni ndogi ikilinganishwa na kazi 946 zilizowasilishwa 2012.

Alibainisha katika kazi zilizowasilishwa mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwasilisha kazi 500, Mwanza 103, Arusha 59, Zanzibar 57 na Kagera 23.


Naye Rais wa MCT, Jaji Robert Kisanga, alitoa pongezi kwa majaji walioapishwa na kuwaasa kufanya kazi kwa moyo wa kujitolea na bila kuwa na upendeleo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.