Na Mwanajuma Mmanga
RAIA wa Italia, Caborn Michael (35), amefariki
dunia katika bahari ya Matemwe mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati akiogelea akiwa
na chombo baada ya kupigwa na mawimbi.
Mwili wa marehemy ulifikishwa hospitali ya
Mnazimmoja kwa uchunguzi.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Kaskazini Unguja, Hassan Muhammed Masangi, alisema, marehemu ambae
alikuwa mtalii, alifikia hoteli ya Waridi iliyopo Matemwe tangu Januari 22
akiwa pamoja na mkewe alietajwa kwa jina la Monica Bars.
Alisema mwili wake ulipatikana Januari 28 katika
ufukwe wa hoteli ya Mapenzi Village iliyopo
Pwani Mchangani na chombo alichokuwa akitumia kiliokotwa Kiwengwa.
Aliwataka watumiaji wa bahari kuwa waangalifu
hasa katika kipindi hichi cha upepo.
No comments:
Post a Comment