Habari za Punde

BREAKING NEWSS:::Lori la Mafuta Lapinduka katika Mlima Sekenke na kuwaka Moto na Kuuwa Watu Wanne Joni hii.



Baadhi ya Wananchi waliofika katika ajali hiyo wakiangalia mabaki ya Lori hilo baada ya kupata ajali na kuwaka moto leojioni likiwa katika safari zake za kusafirisha Mafyta nje ya Dar-es-Salaam, kupeleka mkoa wa jirani..
Mabaki ya Lori hilo baada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii, baada ya kupata ajali katika eneo la mlima sekenke.
                                  Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii

                                 Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeunguaa
                                                  Hii ni njia ya mlima sekenke

Lori la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya sekenke mkoani Singida na kuua watu wanne hapohapo.Chanzo cha ajali hiyo ni breki kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima huo.Shuhuda wa ajali hiyo bwana Julius Chacha alipoongea na mtandao wetu wa Dj sek blog amesema kwamba Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.Akiendelea kuongea shuhuda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kuwa moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.Watu wanne wamekufa papo hapo kutokana na ajali hiyo.Polisi walikuwa bado hawajafika eneoo la tukio mpaka tunaondoka eneo la tukio.

1 comment:

  1. Jee Watanzania mwahisi lifanyike lipi kuepuka vilio kama hivi Tz au tuendelee kuyafumba macho yetu tu tukiachilia wanaokufa barabarani waendelee kufa, wapatao ulemavu nawapate au mali kupotea nazipotee au tufanyeni nini. Hivi kweli Watanzania sote wenye akili timam ,ndio tusilijuwe lakufanya! Yasikitisha sana.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.