Na
Kija Elias, MOSHI
BENKI
ya Damu imezionya hospitali zenye tabia ya kuwauzia damu wagonjwa.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Meneja wa kituo cha damu salama  kanda ya kaskazini, Dk. Wilhellmuss  Mauka, 
wakati wa zoezi la uchangiaji damu kwa hiari kutoka kwa vijana zaidi ya
50 wa kanisa la Waadventista Wasabato Majengo manispaa ya Moshi mkoani
Kilimanjaro.
Alisema  kuna  urasimu unaofanywa na baadhi ya watendaji wa
hospitali kuchukua fedha kutoka kwa wagonjwa ambao wamepungukiwa damu kitendo
ambacho ni kinyume chaa maadili ya uuguzi.
“Ni
kweli kuna baaadhi ya hospitali zimekuwa zikiwauzia wagonjwa damu, kitendo hiki
ni kibaya, damu siyo kitu ambacho anaweza akapewa kila mgonjwa mwenye upungufu
wa damu,  na upatikanaji wake sio kwa
fedha,” alisema.
Alisema
katika hospitali kuna maalumu wanaokabidhiwa chupa za damu lakini cha
kushangaza wamekuwa wakiuza kwa wagonjwa, tena kwa fedha nyingi.
Alisema
serikali imekuwa ikitumia shilingi 225,000 hadi 600,000 kwa ajili chupa moja ya
damu ikiwani ni pamoja na  kuzikusanya na
kuzifanyia tafiti, lakini cha kusikitisha watu hao wasio waaminifu huuza kwa
shilingi 20,000.
Aliwashukuru
 vijana wa Sabato walioonesha nia ya
kujitolea damu na kusema mchango wao utasaidia kupunguza upungufu unaoikabili
benki ya damu.
 Kwa upande wake  mzee wa kanisa la Adventista Wasabato Majengo,
Raphael Mseja, alisema bado jamii haijawa na mwamko wa kujitolea katika
kuchangia damu kwa hiari  na kutoa rai
kwa Watanzania kuona umuhimu wa kujitolea ili kunusuru maisha ya mama na
watoto.

damu zote zinauzwa tu tusidanganyane , ukienda hospitali kama hujatoa hongo hupati damu hata kama unachangia hio damu bado watakutoa upepo , hawana huruma wala ubinadamu
ReplyDelete