Na
Mariam Kamgisha,Morogoro
MWENYEKITI
wa Baraza la Taifa la watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (NACOPHA), Vitaris
Makuyula, amesema iwapo dawa za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVs) zitatumiwa
kwa miaka mitatu mfululizo, zinazuia maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa mtu
mwengine.
Alitoa
kauli hiyo mjini Morogoro wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuondoa
unyanyapaa kwa viongozi wa dini na wadau wengine kwa ufadhili wa UNAIDS.
Alisema
maambukizi yamekuwa yakiongezeka kutokana na watumiaji wa dawa hizo kutofuata
masharti ya utumiaji wa dawa hizo.
“Hapa
nieleweke kuwa mtu mgonjwa anaetumia ARV’s kwa miaka mitatu bila kuacha hata
siku moja anaweza kushiriki ngono na mtu asiembukizwa bila kumuambukiza,”
alisema.
Aliwataka
viongozi wa dini kuzungumzia athari za unyanyapaa kwa waumini wao na kuzikemea
pale zinapotokea.
“Nyinyi
viongozi wa dini mna nafasi kubwa ya kukutana na waumini wengi hivyo tunaomba muwe
mstari wa mbele kuhakikisha unyanyapaa unakwisha,” alisema.
Naye mshauri mhamasishaji jamii kutoka shirika la
kimataifa la UNAIDS,Yeronimo Mlawa, alisema unyanayapaa na ubaguzi kwa watu
wenye Ukimwi na dawa za kulevya ni kikwazo kikubwa kumaliza maambukizi mapya.

No comments:
Post a Comment