Na
Mwandishi wetu
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amepokea ujumbe
maalum kutoka kwa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
Ujumbe
huo wa Rais Zuma umewasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini,
Maite Nkoana-Mashabane wakati mama huyo alipokutana na kufanya mazungumzo na
Rais Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam .
Mara
baada ya kuwasilisha ujumbe huo, viongozi hao wamejadili masuala yanayohusu
uhusiano kati ya Tanzania
na Afrika Kusini na masuala ya kikanda ambako nchi zote mbili ni wanachama wa
Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Nkoana-Mashabane
amendoka nchini baada ya kuwawasilisha ujumbe huo.

No comments:
Post a Comment