Habari za Punde

Wawaaaa Jengo la Afisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zenj Hilooo

  Mjengo ukiwa katika maandalizi, utakuwa na Gorofa 10, gorofa mbili ni sehemu ya maegesho ya Magari,kutakuwa na sehemu ya Benk.  
Mjengo huu utakuwa na Ofisi za Mkuu wa Mkoa na sehemu nyegine kwa ajili ya Biashara na gorofa mbili sehemu ya maegesho ya magari.Litakuwa na gorofa 10.  

AFISA Tawala wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ndg, Ayuob Mohammed na Mwakilishi wa Kampuni ya Ex Investments Switzerland Ndg. Razvan Pintilie, wakisaini makubaliano ya awali ya Ujenzi wa Jengo la Kisasa la Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika eneo la Amaan Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Jumba la Wananchi Forodhani

Afisa Tawala wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ndg. Ayuob  Mohammed, akikamilisha taratibu za utiaji wa saini ya makubaliano ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kutakuwa na sehemu nyegini kwa ajili ya kukodisha na biashara.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Zanzibar Joseph Meza, akizungumza katika hafla hiyo ya Utilianaji wa saini ya makubaliano kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na  Kampuni ya Ex Investments Switzerland, itakayojenga jengo hilo. 
Afisa Tawala wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ndg. Ayoub Mohammed, akitowa maelezo ya Jengo hilo kuelezea, baada ya utilianaji wa saini hiyo uliofanyika katika ukumbi wa jengo laWananchi Forodhani Zanzibar.  

Afisa Tawala akizungumza na kutowa ufafanuzi wa ujenzi huo unaotarajiwa kuaza baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kisheria baina ya pande zote mbili.
Chief Operations Officer wa kampuni ya Ex Investments. Ndg. Razvan Pintilie, akizungumza baada ya kukamilisha utiaji wa saini hiyo ya kujenga jengo la kisasa la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika eneo la Amaan 
                            Viongozi wa Osifi ya Mkuu wa Mkoa wakifuatilia utiaji wa saini hiyo.


Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mhe Abdi Mahmoud akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya utilianaji wa saini ya ujenzi wa Jengo la Kisasa la Gorofa 10 kwa ajili ya Ofisi yaMkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi.

3 comments:

  1. maendeleo ya nchi hayapimwi kwa magorofa au majengo , bali kwa huduma za kijamii kama maji , umeme , elimu na afya , hivi vyote nilivyovitaja mpaka leo miaka zaidi ya nusu karne yamekushindeni kwa nchi ambayo idadi ya wakati wake hatuzidi milioni moja na nusu kwa visiwa vyote , huku mnaomba dua , dua gani za kuingizwa moto wa chini?

    ReplyDelete
  2. Jengoo bombaa limetulia likimaliza litaleta madhari nzuri ya zanzibar na inshalah tutazidi kusonga mbele na kama visiwa vya wenzetu duniani

    ReplyDelete
  3. unajua kiasi gani cha fedha za walipa kodi zitatumika kujenga hilo jengo ? unafiri huyo mjenzi anajenga bure? hebu nakuomba utoe laki moja ukampe mtu ambaye humjui kwa kumsaidia ndipo utaona ugumu wa kutoa bila sababu , hawa wanatujengea kwa mkopo bsio buree, na kuna mamilioni yetu yatamezwa na ndugu zetu hao waliosaini hio mikataba , hizo dua wanashukuru mungu kuwapatia ulaji nje nje kama hujui ndugu mchangiaji wa hapo juu na wala hatusongi mbele maisha kwa uchoyo wetu na roho zetu mbaya ikifika ijumaa mbio mbio mstari wa mbele , ikifika ramadhani kufuturisha kwa fedha za haramu , hatutoendelea imemwagika damu ya watu wasio na hatia wakati wa mapinduzi , maendeleo yatakuja kwa kuvunja muungano na watawala waliopo wakubali kuwa walidhulumu nafsi za watu , watubu . Kwa mchangiaji wa pili mandhari mazuri hayaleti manufaa kwa umma , nakubaliana na mchangiaji no.1 kuimarishwa kwa huduma za jamii ndio maendeleo.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.