Habari za Punde

Dkt. Shein Azinduzi wa Nembo ya Miaka 50 ya Muungano Bwawani Hoteli Zanzibar

Nembo ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania iliozindulia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, sambamba na Uzinduzi wa sherehe za Miaka 50 ya Muungano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. 



Wasanii wa Kikundi cha Big Star wakitowa burudani katika hafla hiyo ya Uzinduzi wa sherehe na Nembo ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapnduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiponyeza kitufe kuashiria kuizinduwa Nembo ya Miaka 50 ya Muungano, katika ukumbi wa Salama Bwawani, kulia Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kushoto Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, wakishuhudia uzinduzi huo.

Viongozi wa Meza Kuu wakiwa katika hafla hiyo.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. AliMohamed Shein, akihutubia mkutano huo wa Uzinduzi wa Nembo ya Miaka 50 ya Muungano katika ukumbi wa hotele ya Bwawani.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akizungumza katika hafla hiyo ya Uzinduzi wa sherehe za Muungano na Nembo ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud, akitowa maelezo ya hafla hii ya Uzinduzi katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
Wananchi waliohudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dkt Shein akihutubia 




 


5 comments:

  1. Kwani sisi sio kama hatuutaki tu, lakini kila tukitizama manufaa hatuyaoni, halafu munatwambia tukienzi kitu ambacho hakina faida sasa sijui mnatufikiria vipi, mfano mfanya biashara kaleta bidhaa haitoki (haimuingizii faida) halafu ang'ang'anie kuleta bidhaa hiyo hiyo, mtu huyo atakua vipi? na sisi msitufanye hatuna akili.

    ReplyDelete
  2. Hatuhitaji nembo,tunahitaji uzinduzi wa MKATABA wa Muungano waliotiliana sahihi.

    ReplyDelete
  3. Inna lillahi wa Inna ilyhi raajiuwn,basi nyie ni sherehe tu na kutizama wanawake wakikata viuno.Zina ina anzia hapo na macho yenu watakuja kukutoleeni ushahidi siku ya hukmu,oneni raha Duniani leo laniki kesho ni majuto.

    ReplyDelete
  4. mnaopenda kuvunja muungano nadhani hamjui kitakachotokea unguja na pemba ambapo kila kisiwa kitataka kiwe na dola yake na pia hamsomi alama za nyakati kwa migogoro inayowakuta majirani zetu,using'ang'ania kuvunja muungano bila kufikiria kijacho kuwa ni ghalama kubwa kwa maisha yako.
    Emma James

    ReplyDelete
  5. Wararaweeeee! Mdau wa nne ujuwe moja,hatuombi litokee lakini likitokea ujuwe ni nafuu kubwa sana kwa Unguja,upo hapo.Maana ngawira zitakuwa nyingi. Mali isiyohamishika sikwambii tena.Temea mate chini lisitokee.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.