Msanii wa Kizazi Kipya Chaby Six akitowa burudani katika onesho hilo lililofanyika katika viwanja vya Michezani Kisonge Zenj, na kutowa burudani kwa Wasanii wa Zenj na Bongo.
Msanii Chaby Six akifanya vitu vyake katika Tamasha hilo viwanja vya kisonge.
Msanii Mwansiti akiwa katika jukwaa katika tamasha hilo la EZY PESA CONCERT & BAZAAR. katika viwanja vya kisonge michezani Zenj.
Master J, akipiga picha kupitia simu yake ya mkononi kuchukuwa kumbukumbu ya tamasha hilo lililobagawisha Vijana wa Zenj, katika viwanja vya kisonge michezani.
Jaji Master J akiwasalimia Wapenzi wa miziki wa Kizazi Kipya wakati wa Tamasha la EZYPESA CONCERT & BAZAAR, lililofanyika katika viwanja vya kisonge michezani.
Hapo sasa wakati Msanii Shaa akiimba wimbo wake Saga saga katika tamasha hilo lililofanyika katika viwanja vya Kisonge.
Hapo sasa lete vitu ndivyo inavyoonekana akisema msanii Shaa alipokuwa akilishabulia jukwaa katika onesho la EZYPESA CONCERT & BAZAAR ndani ya Zenj viwanja vya Kisonge michezani.
Msabiki wa muziki wa Kizaji Kipya akiwa jukwaani na Msanii Shaa akitowa burudani nae. katika onesho hilo.
Huu ni upotoshaji, ufuska na njia moja ya kufundisha maadili mabovu kwa vijana wetu. Angalia vijana wetu wadogo maskini walivyojana kusikiliza na kuoneshwa upotofu. Halafu utasikia vijana wanaharibika, kwanini wasiharibike wakiti kila pembe ya maisha yake ameandaliwa mazingira ya kumpotosha.
ReplyDeleteHii tabia ya kutafuta mashangingi na mafuska kutoka Tanganyika kuja zanzibar kuleta upotofu ina lengo la kuondosha kabisa zile silka za wazanzibari zenye maadili mema.
Hivi serikali kutipia wizara ya vijana hailioni hili. Hii tabia ya kuleta matamasha yenye kuchochea maovu kwanini haipigwi marufuku?? au ndio kudumisha muungano??
Tujue tu twendako si mbali na kila mtu ataulizwa kwa alichokucha. Serikali (kwa maaana ya viongozi) wataulizwa vipi waliwasimamia watu wao katika mwendendo mwema na maadili mazuri.
Mimi nakumbusha tuu.