NaJumbe
Ismailly,IRAMBA
PAMOJA
na kukamilika miundombinu ya maji tangu mwaka 1998, zaidi ya wakazi 1000
wanaoishi katika kaya 335 zilizopo kijiji
cha Meli,tarafa ya Kisiriri wilayani Iramba,mkoani Singida,hawana huduma ya
maji safi na
salama kwa zaidi ya miaka hamsini sasa.
Hayo
yamebainishwa na wananchi wa kijiji hicho kufuatia uchunguzi uliofanywa na
shirika moja lisilokuwa la kiserikali linalojishughulisha na uboreshaji wa afya
la Health Actions Promotion Association (HAPA) la mkoani Singida kutaka
kufahamu sababu za wananchi hao kutokuwa na huduma hiyo.
Wakizungumza
kwa jazba na kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema tangu mwaka 1978 tanki
la maji pamoja na miundombinu ya maji ilipokamilika kujengwa, Idara ya maji
wilaya,imeshindwa kupeleka mashine ya kusukuma maji iliyokuwepo kwa kile
ilichodai imeibiwa.
Baadhi
ya wananchi hao, Shiguna Shiguna,ambaye pia ni Ofisa kilimo na maendeleo ya mifugo
wa kijiji cha Meli, alismea wananchi
wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la maji tangu walipopata uhuru.
Kwa
mujibu wa mtumishi huyo wa serikali pamoja na kuwepo wakuu wa idara ya maji na
kuhudhuria mikutano ya kijiji,walikuwa wakitoa majibu ya kuwa wapo njiani na
haijafahamika mpaka sasa ni njia ipi waliyopitia.
Naye
mmoja wa wajumbe wa nyumba kumi katika kijiji hicho,Maria Kitundu, aliyeonekana
kuguswa zaidi ya tatizo hilo , alisema kutokana
na tatizo hilo
wamekuwa wakilazimika kutoka saa 11:00 alfajiri kwenda kutafuta maji.
Hata
hivyo, mwanamama huyo aliweka bayana kwamba pamoja na kutoka usiku lakini waume
zao hawajali umbali uliopo na uchache wa maji hivyo wanapochelewa kurudi
nyumbani hufuatwa na waume zao na kupigwa.
Naye
John Pyuza, alisema licha ya kijiji kufungua akaunti ya maji baada ya viongozi
kutoka wilayani kufika kijijini hapo na kuwahamasisha juu ya kuwapelekea huduma
hiyo, bado maji yameshindikana.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la HAPA mkoani Singida, David Mkanje,
alisema kupitia shirika la World Vision Tanzania linalofadhili mradi huo,katika
wilaya za Singida vijijini na Iramba mkoani Singida na Nzega,mkoani Tabora zilizopo
katika mradi wa ufuatiliaji na uwajibikaji jamii (SAM),kati ya shilingi bilioni
30 zilizotengwa kwa ajili ya kusambaza huduma ya maji safi na salama katika
wilaya hizo, shilingi bilioni 23 zimeshatumika na kwamba mradi huo unatarajiwa
kukamilika ifikapo Oktoba.
Akizungumzia
hoja ya wananchi,Mhandisi wa maji wa wilaya ya Iramba, Eng.Leonidas Rweyemamu,
alisema licha ya kutoikubali taarifa ya shirika hilo pamoja na malalamiko ya wananchi,alisema
taarifa zilizotolewa hazina ukweli wowote.
Muda wa miaka 50,jee wamepita wabunge wangapi katika wilaya hiyo? Jee serikali za walaya,tarafa na serikali ya mkoa hivi haijapata taarifa ya usumbufu huo.Jee kwa miaka 50 serikali ya kijiji imeshindwa kukipatia kijiji mashine iliyoibiwa na huduma kurudi au kuanza mara moja .Iko namna ,semeni jengine.Maana kwa hili haliingii akilini.
ReplyDelete