Na Joseph
Ngilisho,ARUMERU
DIWANI
wa kata ya Olkiding'a,Samweli
Ngarabani,amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kuwatolea majibu machafu kwenye mkutano wa
hadhara aliouitisha kwa lengo la kuhamasisha uchangiaji wa mradi wa ujenzi wa
maabara katika skuli ya sekondari
Olkiding'a.
Tukio
hilo lilitokea mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Olgoruno,Olkidinga,wilayani
Arumeru,baada ya kuwataka wananchi hao kuchangia shilingi 60,000 kila mmoja,kiwango
walichodai ni kikubwa ikilinganishwa na
hali zao za maisha.
Hali
hiyo ilisababisha vurugu kubwa kutoka kwa wananchi hao na baadhi yao kutaka kumshambulia
kwa siraha.
Kilichowakasirisha
wananchi hao ni baada ya mmoja wa wananchi kuhoji fedha za miradi ya maji na
chumba cha kompyuta alizowachangisha kipindi cha nyuma huku wakimhoji kwanini
amekuwa akiibuka tu wakati wa michango na baadae haonekani katika kata hiyo,kusikiliza
kero za wananchi.
Diwani
huyo alijinasibu kwa kutamka kuwa watake wasitake lazima wachangie maendeleo ya
kata hiyo huku akitamba kuwa ameagizwa
na rais kusimamia michango hiyo na kuwatisha kuwa iwapo mwananchi yeyote
atakayekaidi agizo hilo
atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.
“Mkikataa
mimi sitishwi na hilo na suala la maendeleo ni lazima mtachangia mtake
mstake,tutawachukulia hatua za kisheria ,hili ni agizo la rais Kikwete,”
alisema.
Kauli
ya diwani huyo ilionekana kuwaudhi na kuwatia hasira wananchi hao ambapo baadhi
ya vijana walianza kumzonga wakimtaka aondoke kwenye kata hiyo,huku wengine
wakinyanyua silaha za jadi wakimtishia kumkatakata,lakini alilazimika kuwaomba
msamaha kwa kuwapigia magoti huku akiwatuliza wasimdhuru.
Hata
hivyo, mkutano huo kuvunjika baada ya wananchi kuanza kupiga kelele wakidai
hawezi kuchangia chochote mpaka wasomewe mapato na matumizi ya kijiji hicho
wakidai hawakuwahi kusomewa tangu mwaka 2009.
Naye
Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Sarah Mollel, alikiri kutosoma mapato na
matumizi katika kipindi kirefu,hata hivyo alieleza kuwa Mtendaji aliyekuwepo
kabla aliondoka na nyaraka za ofisi hiyo na kwenda nazo kata ya Odonyosambu alikohamishiwa,hivyo
hana kumbukumbu yeyote juu ya mapato na matumizi ya kijiji.
No comments:
Post a Comment