Na
Fatuma Kitima, DAR ES SALAAM
SERIKALI
ya Tanzania
na Japan zimesaini mkataba wa shilingi bilioni 6.02 kwa ajili ya kununua mbolea
ikiwa lengo la kuwasaidia wakulima wadogo.
Hayo
yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha,
Servacius Likwelile.
Alisema
msaada huo utawasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa chakula hasa kwa wakulima
pamoja na kuwainua kiuchumi.
Alisema
pamoja na kuinua kiwango cha mkulima wa chini pia kuwekeza katika miundombinu
hasa masoko ili kuinua sekta ya kilimo nchini.
Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania , Masaki Okada, alisema wameamua kutoa
msaada huo kwa ajili ya kuinua sekta ya
kilimo Tanzania .
Alisema
lengo ni kununua mbolea kwa ajili ya wakulima wadogo ili kuongeza uzalishaji wa
mazao ya kilimo.
Naye
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Dk.Yamungu Kayandabila,
aliishukuru Japan
kwa msaada huo muhimu.
No comments:
Post a Comment