Na
Asya Hassan
JESHI
la Polisi mkoa wa mjini magharibi Unguja, linamshilia Khamis Said Faki mkaazi
wa Kwamtipura kwa tuhuma za kuchoma moto nyumba ya Tatu Makame iliopo Kwamtipura
wilaya ya mjini Unguja, baada ya kumtuhumu kuwa mwanga.
Kamanda
wa Polisi mkoa huo, Kamishna Msaidizi,Mkadam Khamis Mkadam, alisema hayo wakati
akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Muembe Madema.
Alisema
tukio hilo lilitokea Machi 22, baada ya mtuhumiwa akiwa na mwenzake kwenda
nyumbani kwa mwanamke huyo kwa lengo la kuichoma moto nyumba yake.
Alisema
walipofika waliimwagia mafuta ya petroli nyumba hiyo na kuanza kuichoma moto
lakini hata hivyo, moto huo uliwahiwa kuzimwa kabla haujaleta athari kubwa.
Katika
tukio jengine, raia wa Canada, alietambuliwa kwa jina la Christopher Bourvier
Bouker (25) alishambuliwa kwa kuchomwa kisu cha chini ya kitovu akiwa katika
matembezi Darajani.
Alisema
mtuhumiwa alitambuliwa kwa jina la Takadir Khamis, ambae anasadikiwa kuwa na
tatizo la ugonjwa wa akili.
Alisema
majeruhi alikimbizwa hospitali ya Mnazimmoja kwa matibabu na kuruhusiwa baada
ya hali yake kuendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment