Habari za Punde

Maalim Seif: Watanzania wana kila sababu ya kusherehekea miaka 50 ya muungano

Na Hassan Hamad, OMKR.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema Watanzania wana kila sababu ya kusherehekea miaka 50 ya Muungano kutokana na mafanikio yaliyopatikana.
 
Ametaja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni pamoja kuimarika kwa hali ya usalama, ushirikiano na maelewano kwa wananchi wa pande mbili za Muungano.
 
Maalim Seif ametoa kauli hiyo katika hafla ya mkesha wa miaka 50 ya Muungano ilivyofanyika viwanja vya Mnazimmoja jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda.
 
Amesema miaka 50 tangu kuasisiwa kwa Muungano huo ni kipindi kirefu cha kujivunia, ikilinganishwa kuwa nchi nyingi za Afrika zilizojaribu kuungana zimeshindwa baada ya kipindi kifupi cha miungano yao.
 
Hata hivyo amesema Muungano wa Tanzania bado unakabiliwa na kero nyingi zinazohitaji kupatiwa ufumbuzi kwa maslahi ya pande zote mbili na vizazi vijavyo.
 
Hafla hiyo iliyoambatana na urushaji wa fashifashi, ilihudhuriwa pia na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi

3 comments:

  1. Hahahahaaaaaa,mengine yanayoshangaza huangukiwa na vicheko!

    ReplyDelete
  2. Maalim Seif hongera kwa kukaukwa na jeraha la moyo.

    ReplyDelete
  3. maalim seif hauchukii muungano na wala hataki uvunjike anachokipinga ni mfumo wa muungano tanganyika kuvaa koti la muungano hilo tu mkileeka sawa mbona patakuwa hapana malalamiko leo unachukua mafriji unayapeleka bara unachajiwa pesa hata huko ulipolinunua haifiki sjagusa magari nk ukitoa kitu bara kuleta huku unalipia warfege tu kuna usawa hapo

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.