Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete akiwasalimia wananchi wakati alipokuwa alipowasili katika uwanja wa Uhuru katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar ..Pembeni
ni Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
Amiri Jeshi Mkuu Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa
maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru
jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Mohamed Ali Shein wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete akimkaribisha Rais Joyce Banda wa Malawi katika sherehe za miaka 50
ya Muungano.Rais Banda kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya ya uchumi kusini
mwa Afrika SADC.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mfalme MswatiIII katika sherehe za miaka 50 ya Muungano zilizofanyika katika viwanja vya uhuru leo.
Rais dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha
Rais Yoweri Kaguta Museveni katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi katika maadhimisho ya hsrehe za miaka 50 ya Muungano.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta katika hsrehe za miaka 50 ya Muungano(picha na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment