
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa mwendo wa aina yake wakati wa sherehe za miaka 50 ya Muungano.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano ambazo zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Makomandoo kikitoa salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.
Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana bila kutumia nyenzo hapa wakivunja matofali kwa kutumia kichwa na mikono.
Baadhi ya silaha zakijeshi zikipitishwa mbele ya umati kuonyesha uwezo mkubwa wa jeshi letu.
Kikosi cha Wanamaji
Ndege za kivita zikilinda Ndege ya Rais katika maonyesho ya Ndege yaliofanyika kwenye Kilele cha Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano.
Askari wa kikosi cha Mwamvuli akishuka kutoka futi 4500 kwenye uwanja wa Uhuru kwenye kilele cha miaka 50.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha mwamvuli .
Maandamano ya WAPANDA .
Matembezi maalum ya kusheherekea miaka 50 ya Muungano .
Njiwa wakirushwa juu kama ishara ya miaka 50 ya Muungano ambapo watu waliorusha njiwa hao nao wametimiza miaka 50.
kwani kuna vita nini? naona maonyesho ya kijeshi zaidi kuliko sherehe za muungano , au ndio mnatuonyesha tusiotaka muungano kuwa mtatumia mabavu kututawala? Huoni kuwa hio ni asili ya udikteta JK , pia kusema wataochezea muungano watakiona cha mtema kuni , jee una uhakika utaishi milele hutokutana na bingwa wa mabingwa , mfalme wa wafalme , mtukufu wa watukufu? unao muda JK rudi kwa mola kabla ya kukufika umauti kama firauni alivyoomba msamaha wakati umauti umemfika Mtukufu mungu akamjulisha muda wa kuomba msamaha umekwisha yupo kwenye kisago mpaka leo , cheo mara nyingi humfanya binadamu kuwa na kiburi na jeuri , usijisahau ndugu yangu JK rudi kwa mola uombe msamaha wa nguvu , utuachie visiwa vyetu tena babaa tushachoka kutawaliwa , hayo majeshi na vifaa mlivyonavyo havitushughulishi hata kidogo labda kama ulikuwa unawaonyesha majirani zako uganda na kenya na malawi , hao ndio tishio kuliko zanzibar ambayo imetanganishwa na bahari , nashangaa husema kuwa znz ni tishio ikiwa huru , wakati nchi mlizopakana nazo hamuoni tishio vipi uone tishio kisiwa kiko maili kadhaa mbali na ufukwe wa tanganyika ,watu wake hawazidi milioni moja na nusu?
ReplyDeletemhe JK usitutishe hatuutaki muungano hauna faida yoyote tushachoka musitulazimishe kwanini hamuwaulizi waznz kama wanautaka au laa?
ReplyDelete