Na Fatina Mathias, Dodoma
Wanachama wa CCM waliokisaliti chama wakati wa
uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga na Chalinze watachukuliwa hatua.
Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama
hicho Tanzania Bara, Philip Mangula, katika hafla ya kuwapongeza Mbunge wa
Chalinze, Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Kalenga, Godfrey Mgimwa.
Alisema kwa mujibu wa kanuni za CCM kosa kubwa
kuliko yote ni kwa mwanachama kukisaliti chama hicho kwa kushirikiana na upinzani
kwa lengo ya kukiweka katika hali ya kushindwa.
Alisema watachukua hatua kwa wanachama wote
walioshirikiana na upinzani kupinga uteuzi wao na kwamba makatibu kata wanajua
hatua zitakazochukuliwa.
Aliwataaka wabunge hao kuepuka makundi ndani ya
majimbo yao kwa
kuwa kanuni za CCM zinapiga marufuku kwa
kiongozi kujenga makundi yanayoweza kuvunja umoja ndani ya chama.
Aidha, alipiga marufuku kwa mwanachama yeyote
kusogeza pua yake kwa nia ya kuanza kupiga kampeni katika majimbo hayo ambayo
tayari yana wabunge.
Alisema wabunge hao waachwe wafanye kazi zao
katika kipindi hiki kilichobaki na kwamba wanachama wanaruhusiwa kutangaza nia
lakini ni marufuku kuanza kampeni.
“Marufuku kutangaza nia kabla ya wakati, muda wa
kampeni utatangazwa rasmi, makatibu wa wilaya
simamieni hili, atakayefanya kampeni kabla ya wakati mwekeni katika
kumbukumbu ya uhalifu,” alisema.
Alisema ni marufuku kwa mwanachama asiye kiongozi katika eneo husika kutoa
msaada, mchango au zawadi katika eneo analokusudia kugombea.
Kwa upande wake, Ridhiwani alisema CCM imemlea tangu
akiwa na miaka minne na kuahidi hatakiangusha chama hicho.
Naye Mgimwa aliahidi kufanya kazi ya ubunge kwa
maslahi ya taifa na jimbo la Kalenga.
Hawa Ma-CCM sasa naona Wamekua kama Makaburu , Kazi zao Vitisho Tuuu. Anaekisaliti Chama atashuhulikiwa, weee atashuhulikiwa wee. Kwa nini musijiulize nyinyi Wakuu wa CCM kuna Dosari gani ndani ya CCM na muweze kukaa chini muikosowe baada yakuwatisha Wananmchi waliokua wana itikadi tofauti na zile za kwenu ambazo ni za Kidiktetor...?
ReplyDeleteKwanini anaekisaliti chama asifukuzwe halafu mukamuweka mtu mwengine.. Nyintyi Miongozi ya Africa ni Mijinga kweli kweli.. Wao Na Kuabudu Chama tuu hata kama Itikadi zake haziendani tena na wakati tulionao wao bado wamengangania tu mpaka Nchi waitumbukize kwenye Vita vya wenyewe kwa wenyewe...
Tunataka kuona Serikali ya Tanganyika na Zanzibar inapata Utawala wa Chama chengine ili tuone kama wataweza kuleta maendeleo kwa jamii...
Miaka 50 sasa CCM iko madarakani na hakuna cha maana walichokifanya labda kula hela ya Umma..
kabisa kabisa, huwa wanahubiri demokrasia lakini vitendo vyao ni vya kishenzi vya zamani za kale ambapo watu walikuwa wakitumia nguvu na kulazimisha mambo kwa kuwa uweleo wao ulikuwa mdogo , lakini naona sasa tunarudi kule kule ushenzini japokuwa tupo karne ya 21 , watu wanashindwa kushindana kwa hoja. Kuna haja ya kuingiza ushindani wa kutumia maneno mashuleni ( debate ) ili watoto wetu wawe mahiri na kuelewa kubishana kwa kutumia lugha nzuri
ReplyDelete