UMOJA
wa Ulaya (EU) umekubali kuisaidia Zanzibar katika upatikanaji wa nishati ya
umeme, inayotokana na nguvu za jua na upepo.
Mradi
huo mkubwa wenye thamani ya shilingi bilioni 6.8, utatekelezwa kwa kipindi cha
mwaka mmoja, chini ya Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), lenye dhamana ya
kuwasambazia umeme wananchi wa Zanzibar .
Mradi
huo utahusisha masuala ya utafiti na utekelezaji wa mradi huo, hadi nishati
hiyo itakapopatikana ambayo kwa kiasi kikubwa itasaidia kupunguza utegemezi wa
umeme.
Akizungumza
katika hafla ya utiaji saini utekelezaji wa mradi huo, Balozi wa Umoja wa
Tanzania na kanda ya Afrika Mashariki, Filiberto Ceriani Sebregondi, alisema
lengo la mradi huo ni kukuza maendeleo endelevu na kupunguza umaskini kwa
wananchi wa Zanzibar .
Alisema
mradi huo unatekelezwa kutokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya Zanzibar na Umoja huo
uliodumu kwa muda mrefu sasa.
Alisema
mradi huo utaleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa Zanzibar na wananchi wake.
Aidha
alisema, EU itaendelea kuisaidia Zanzibar na Tanzania kwa jumla katika sekta
mbali mbali za kiuchumi, ambapo kuanzia mwaka huu hadi 2020 umoja huo utatoa
dola za Marekani milioni 626.
Nae
Waziri wa Fedha, Omar Yussuf Mzee, aliipongeza EU kwa kusaidia sekta ya nishati
ili kuhakikisha Zanzibar
inakuwa na vyanzo vyake vya umeme.
Aidha
aliishukuru EU kwa kuendelea kuiunga mkono Wizara ya Fedha, katika utekelezaji
wa mipango mbalimbali ya kiuchumi kwa faida ya nchi na wananchi wake.
Nae
Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati, Ramadhan Abdalla Shaaban,alisema
mradi huo utasaidia kasi ya upatikanaji wa nishati ya umeme, ambapo kwa muda
mrefu Zanzibar
imekuwa ikichukua juhudi kuhakikisha inapatikana.
Katika
hatua nyengine, EU imesaini mkataba wa kuzisaidia asasi mbali mbali za kiraia
(NGO’s) zilizochini ya mwamvuli wa ANGOZA zinazoshiriki katika utetezi wa haki
za binaadamu.
Mradi
huo wa miaka mitatu, utasaidia kupunguza kasi ya udhalilishaji wa wanawake na
watoto, kupunguza tatizo la ajira kwa watoto, kuimarisha demokrasia na utawala
bora na kulinda haki za binaadamu na usawa wa kijinsia.
Mradi
huo wenye thamani ya shilingi bilioni 6.8 utatekelezwa Unguja na Pemba .
Akizungumza
katika hafla hiyo, Waziri wa Sheria na Katiba, Aboubakary Khamis Bakary,
alisema asasi zitakazofaidika na fedha hizo ni zile zinazofanya shughuli zake
na ambazo zimepata usajili kwa mujibu wa sheria.
Mwenyekiti
wa ANGOZA, Asha Aboud Mzee, alisema msaada huo umeweka uhusiano mwema kati ya
NGO’s, serikali na Umoja wa Ulaya na kwamba ni faraja kubwa kwa asasi za kiraia
nchini.
Katika
mkataba wa radi wa nishati ya umeme, serikali iliwakilishwa na Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha, Khamis Mussa Omar na mradi wa kusaidia NGO’s serikali
iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Juma Ameir Khafidh.
No comments:
Post a Comment