Na Amina
Omari,Tanga
Serekali ya
Mapinduzi ya Zanzibar ipo kwenye hatua za mwisho za kupitisha sheria ya adhabu
ya kuitumikia jamii kwa watoto wenye umri wa miaka 18, wanaopatikana na hatia
na kuhukumiwa vifungo.
Hayo yamaeelezwa
na Mkurungezi wa Maendeleao ya Wanawake na Watoto, Rahma Ali Khamis,wakati akizungumza kwenye ufungaji
wa mafunzo kwa wakufunzi wa kitaifa kuhusiana na malezi kwa familia kuzuia
ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika jijini Tanga.
Alisema
kukamilika kwa sheria hiyo kutatoa mwanya kwa watoto kurekebishwa tabia zao na
jamii badala ya kuwachanganya kwenye magereza ya wakubwa.
Alisema
katika kukabiliana na tatizo la ukatili kwa watoto na wanawake hatua mbalimbali
zimeanza kuchukuliwa ikiwemo kutoa elimu kuhusu madhara ya vitendo hivyo pamoja
na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria watuhumiwa wa vitendo hivyo.
Aliongeza
kuwa kuanzisha mahakama za watoto ambazo zina mahakimu wake na wanasheria wake
kumesaidia kuleta msaada wa kisheria kwa watoto hao.
Nae Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Anna Maembe, ambaye
alikuwa mgeni rasmi, aliviagiza vyuo vya maendeleo ya jamii pamoja na vyuo vya wananchi
kuingiza kwenye mtaala masula ya elimu ya malezi ili wanafunzi wanaomaliza
watoke na uwelewa kuhusu jinsi ya kuzuia ukatili.
Alisema
mitaala hiyo itasaidia kupunguza tatizo la unyanyasi wa kijinsia wanaofanyiwa
watoto katika maeneo mbalimbali kwani elimu hiyo itawafikia watu wengi katika
jamii hususani madhara ya ukatili huo.
No comments:
Post a Comment